top of page

WATU 66 WAFARIKI 55 WAJERUHIWA BAADA YA MOTO KUTEKETEZA HOTELI YA KIFAHARI UTURUKI

Na VENANCE JOHN


Moto umeteketeza hoteli moja ya kifahari katika eneo la mapumziko la Uturuki la Bolu na kusababisha vifo vya watu 66 na wengine 51 kujeruhiwa. Moto ulizuka katika Ghorofa 12 ya hoteli kwa jina la Grand Kartal majira ya saa 03:27 kwa saa za nchini humo. Majira haya ni wakati wa likizo yenye shughuli nyingi na takriban watu 234 walikuwa kwenye hoteli hiyo.


Idadi ya awali ya watu 10 waliofariki iliongezeka kwa kiasi kikubwa saa chache baada ya moto na wizara ya mambo ya ndani ya Uturuki ilisemema takriban watu wawili walikufa baada ya kuruka kutoka kupitia madirisha ya hoteli hiyo. Picha zinazosambaa nchini humo zinaonyesha kitani kikining'inia kwenye madirisha ambayo ilitumiwa na wale wanaojaribu kutoroka jengo lililokuwa likiungua.


Gavana wa jimbo la Bolu Bw. Abdulaziz Aydin amesema ripoti za awali zilidokeza kuwa moto huo ulizuka katika sehemu ya mgahawa uliopo ghorofa ya nne ya hoteli hiyo na kusambaa hadi sakafu ya juu.


Hoteli hiyo ilikuwa ikichunguza iwapo wageni walikuwa wamenaswa kwenye vyumba vyao moto huo ulipokuwa ukienea. Juhudi za uokoaji zilikuwa zinaendelea hadi asubuhi, na waziri wa mambo ya ndani amesema huduma za dharura zimetuma watu 267 kupambana na moto huo.

Коментарі


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page