Na Ester Madeghe,
Polisi nchini Ujerumani wamewakamata washukiwa 8 wa kundi la wanamgambo wa mrengo wa kulia wanaoamini kwenye ubaguzi wa rangi, waliokuwa wanafanya mazoezi ya vita kwa ajili ya kuipindua serikali ya Ujerumani.

Katika taarifa iliyotolewa leo, waendesha mashtaka wa shirikisho wamesema washukiwa hao ni sehemu ya shirika lililoundwa Novemba mwaka 2020 linaloitwa "Saechsische Separatisten" au wanaotaka kujitenga kutoka jimbo la Saxony.
Miongoni mwa waliokamatwa ni washukiwa 4 waasisi wa kundi hilo, saba kati yao wamekamatwa katika miji ya mashariki mwa Ujerumani ya Leipzig, Dresden na Meissen.
Commenti