top of page

WATU NANE WANAODAIWA KUMBAKA MTALII MBELE YA MUME WAKE WAKAMATWA

Huu ni muendelezo wa taarifa tuliyokupasha siku chache zilizopita juu ya mwanadada aliyebakwa mbele ya mumewe.

Sasa Polisi nchini India wamewakamata watu nane kuhusiana na shambulio na ubakaji wa



genge la wanablogu wawili wa Uhispania wanaotumia pikipiki kusafiri maeneo mbalimbali (Mke na Mume) mwishoni mwa wiki iliyopita katika jimbo la Jharkhand mashariki.

Polisi walisema waliwapata wawili hao ambao ni mume na mke siku ya Ijumaa jioni katika wilaya ya Dumka jimbo ambapo wanandoa hao walikuwa wamepiga kambi. Polisi walisema wawili hao walionekana kana kwamba walikuwa wamevamiwa. Walipopelekwa katika hospitali ya eneo hilo, mke alimwambia daktari kwamba alibakwa.

Awali watu watatu walikamatwa Jumamosi, na, katika mkutano na wanahabari Jumatatu, polisi walitangaza kuwa wamewakamata wanaume wengine watano kuhusiana na tukio hilo.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page