top of page

WATU WAKOSOA WAZIRI MKUU WA BANGLADESH KULIA BAADA YA KITUO CHA TRENI KUHARIBIWA NA MAANDAMANO...

Na VENANCE JOHN


Waziri mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina ameshutumiwa kwa kulia machozi yaliyotafsiriwa na wengi kuwa ya uongo baada ya kupigwa picha akilia kwenye kituo cha treni ambacho kiliharibiwa wakati wa maandamano ya kupinga mfumo wa ajira wa serikali. Mtandaoni, wengi walimshutumu Bi Hasina kwa kutoonesha kiwango sawa cha huruma kwa waliokufa, au familia zao badala yake akalia kwa sababu ya miundombinu iliyoharibiwa.


Picha hizo zilipigwa wakati wa ziara ya Bi Hasina katika kituo cha treni cha Metro katika jiji la Mirpur siku ya jana Alhamisi, ambapo mashine za kuuza tiketi na kituo cha kudhibiti ishara vilivunjwa. Bi Hasina alipigwa picha akiwa amekunja uso na kujifuta machozi kwa karatasi ya tishu.


             Takriban watu 150 wameuawa kutokana na maandamano ya nchi nzima ambapo makabiliano makali kati ya polisi na wanafunzi wa vyuo vikuu yakitokea, huku vikosi vya usalama vikituhumiwa kwa kutumia nguvu kupita kiasi. Waandamanaji wamekuwa wakitaka mfumo wa upendeleo wa nafasi za kazi serikalini kufutwa jambo ambalo tayari limeshatekelezwa na mahakama ya juu nchini humo kwa kubadili mfumo huo wa ajira.


             "Ni aina gani ya mawazo inawaongoza kuharibu vituo vinavyorahisisha maisha ya watu? Jiji la Dhaka lilikuwa limejaa msongamano wa magari. Reli ya Metro ilitoa ahueni. Siwezi kukubali kuharibiwa kwa kituo hiki cha usafiri kilichotengenezwa kwa teknolojia ya kisasa," gazeti la kila siku la Bangladeshi The Business Standard lilimnukuu waziri mkuu wakati akizungumza.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page