top of page

WATU WAWILI WAFARIKI BAADA YA NDEGE KUGONGANA...

Kutoka nchini Kenya Watu wawili waliokuwa ndani ya ndege aina ya Cessna mali ya Ninety-Nines Flying School ambao ni Rubani Mwanafunzi na Mkufunzi, wamefariki dunia baada ya kugongana na ndege nyingine angani jijini Nairobi.



Ndege hiyo ilianguka katika Mbuga ya Kitaifa ya Nairobi, na kuwaua wawili hao papo hapo.

Ndege ya pili, waliyogongana nayo ni Dash 8, mali ya Safarilink Aviation Limited, ambayo imethibitisha kuwa ilikuwa ikielekea Diani, ikiwa na abiria 39 na wafanyakazi 5 hata hivyo hakuna aliyejeruhiwa katika ndege hiyo.

Wafanyakazi wa ndege hiyo waliamua kurejea mara moja kwenye Uwanja wa Ndege wa Nairobi-Wilson kwa ukaguzi na tathmini zaidi na walitua salama.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (KCAA) tangu wakati huo imeanza uchunguzi kubaini hali iliyosababisha ajali hiyo ya angani.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page