top of page

WATUHUMIWA 13 WAKAMATWA KWA KUCHOMA BASI MOTO KOROGWE

WATUHUMIWA 13 WAKAMATWA KWA KUCHOMA BASI MOTO KOROGWE


Jeshi la Polisi Mkoani Tanga limesema mpaka sasa limefanikiwa kuwakamata Jumla ya Watuhumiwa kumi na tatu (13) kuhusiana na tukio la kuchoma Basi aina ya Scania lenye namba za usajili T.668 mali ya Kampuni ya Sai Baba, katika Kata ya Msambiazi, Tarafa ya Korogwe, Wilaya ya Korogwe Februari 27, 2024.

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Almachius Mchunguzi wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake na kusema Mara baada ya Upelelezi kukamilika watuhumiwa hao watafikishwa Mahakamani.

Comentarios


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page