top of page

WATUHUMIWA 17 RAIA WA ETHIOPIA, MBARONI KWA KUINGIA NCHINI BILA KUFUATA TARATIBU...

Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara April 07, 2024 wamethibitisha kuwakamata watu 17 raia


kutoka nchini Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini bila ya kufuata utaratibu ikiwemo kutokuwa na vibali.

Akizungumzia tukio hilo ofisini kwake, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Lucas Mwakatundu amesema watuhumiwa hao wamekamatwa Kijiji cha Kiongozi, Kata ya Maisaka, Tarafa ya Babati, Wilaya ya Babati, wakiwa wanasafirishwa kwenye gari aina ya V8 VXR yenye namba za usajili STL 1964Mwakatundu amewaomba wananchi na jamii kwa ujumla kushirikiana na Polisi katika kuhakikisha hakuna magendo yanayopitishwa kwa kutoa taarifa za watuhumiwa wa uhalifu

Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara pia limewaonya Watanzania na wasio wazawa kuacha mara moja kujihusisha na usafirishaji wa magendo ikiwemo wahamiaji haramu, dawa za kulevya na nyara za serikali.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page