top of page

WAZIRI MKUU MAJALIWA ASHIRIKI KONGAMANO LA WANAHABARI WA MITANDAO YA KIJAMII

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Mei 21, 2024 ameshiriki katika kongamano la Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) akiwa kama mgeni rasmi.

Katika Kongamano hilo, liliojadili kuhusu miaka mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Madarakani pamoja na Uhuru wa Vyombo vya Habari Waziri Mkuu Majaliwa amesema




"Ninawapongeza sana wanahabari kwa kazi nzuri mnayoifanya katika kuwahabarisha wananchi, kusambaza taarifa, na kuelimisha jamii kupitia mitandao ya kijamii

Katika kipindi cha miaka mitatu toka Mheshimiwa Dkt. @SuluhuSamia aingie madarakani amewezesha kukua kwa sekta ya habari na hasa ongezeko la watumiaji na wasomaji wa habari kupitia mitandao ya simu Serikali haina namna ya kuwatenganisha Jumuiya hii na Mafanikio ya Serikali yetu. Tunatambua, Tunathamini na tunashukuru kwa kazi nzuri mnayoifanya na endeleeni kufanya kazi kwa uhuru wa kutokiuka taratibu za kitaifa na kimataifa".

"Serikali yetu inatambua na kuthamini jukumu kubwa la vyombo vya habari pamoja na mchango wenu katika maendeleo ya taifa letu

Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa habari za mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vingine kwa ujumla ili kuhakikisha kuwa sekta hii inaendelea kukua na kuchangia katika kuleta maendeleo kwa taifa letu" Amesema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Viongozi wengine walioshiriki katika kongamano hilo ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye pamoja na Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi.

Comentarios


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page