top of page

WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA ATUA TANZANIA KWA ZIARA YA KITAIFA YA SIKU TATU..

WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA ATUA TANZANIA KWA ZIARA YA KITAIFA YA SIKU TATU...

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia, Mhe. Dkt. Abiy Ahmed Ali amewasili nchini leo tarehe 29 Februari 2024 kuanza ziara yake ya kitaifa ya siku tatu.

Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mhe. Waziri Mkuu Abiy amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba.

Mhe. Dkt. Abiy atapokelewa rasmi na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 01 Machi 2024.

Pamoja na mambo mengine ziara ya Waziri Mkuu Abiy inalenga kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Ethiopia katika maeneo ya kimkakati ikiwemo usafirishaji kwa njia ya anga, nishati, kilimo na mifugo, biashara na uwekezaji na Ushirikiano katika sekta za elimu, uhamiaji, na ulinzi na usalama

Ziara hiyo ambayo itakamilika tarehe 02 Machi 2024 inafanyika kufuatia mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page