Waziri Mkuu wa Somalia Hamza Abdi Barre ametangaza kuwa mshahara wake wote wa mwezi Julai atautoa kuwasaidia watu walioathiriwa na mlipuko wa bomu, wiki iliyopita mjini Mogadishu.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_2f29bd44843d442da7f675f5e9301852~mv2.jpg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_2f29bd44843d442da7f675f5e9301852~mv2.jpg)
Pia, mawaziri katika baraza la mawaziri wametangaza kutenga sehemu ya mishahara yao kuunga juhudi za serikali kuwasaidia wahanga wa shambulio la kikatili lililowaua watu wasio na hatia mjini Mogadishu.Baraza hilo la mawaziri limetangaza kwamba serikali imekusudia kutoa dola nusu milioni kwa watu walioathiriwa na mlipuko huo.
コメント