top of page

WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA BANGLASESH ASHITAKIWA KWA MAUAJI, NAYE ASEMA WALIOHUSIKA WAWAJIBISHWE

Na VENANCE JOHN


Waziri mkuu wa Banglasesh aliyejiuzulu Sheikh Hazina hapo jana tarehe 13, Agost 2024, amesema kuwa hatua zinatakiwa kuchukuliwa kwa wote waliohusika na mauaji na uporaji na uharibifu ndani ya nchi hiyo. Kauli hiyo ni ya kwanza tangu kuikimbia nchi yake kufuatia maandamano makubwa yaliyomlazimu kukimbilia nchi jirani ya India.





Kauli ya Bi Hazina imetolewa kwenye mtandao wa X, kupitia kijana wake saa chache tu baada ya mahakama kutoa amri ya kuchunguza namna Sheikh Hazina alivyohusika katika kifo cha mmiliki wa duka la vinjwaji (grocery) wakati wa maandamano. "Watu wengi walikufa kwa kivuli cha jina la mapinduzi mwezi julai", Hazina amesema.


Amesema anataka wale wote waliohusika kwenye mauaji hayo kufanyika uchunguzi wa kutosha na wahusika kutambuliwa kisha kuadhibiwa kisheria. Karibu watu 300 walifariki katika maandamano ambayo yalianza yakipinga mfumo mbovu na wa ubaguzi wa ajira lakini baadaye yakabadili mwelekeo na kumtaka waziri mkuu ang'atuke.


Maafisa kadhaa waliokuwa kwenye uongozi wa Bi Hazina wamekumbana na mashtaka ya jinai, akiwamo aliyekuwa waziri wa sheria Anisul Huq na mshauri wa Bi. Hazina, Salman F. Rahman kwa kuchochea kuuliwa kwa watu wawili.


Pia kesi inayomlenga moja kwa moja Bi Hazina mwenyewe imefunguliwa na Amir Hamza, ambapo mwanasheria wa Hamza, Anwarul Islam amesema kwamba baada ya mahakama kupitia kesi hiyo, polisi wameagizwa kuanza uchunguzi.


Wengine waliojumuishwa kwenye kesi hiyo ni Obaidul Quader ambaye ni Katibu mkuu wa chama cha Bi. Hazina cha Awami League Party, aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi hiyo wakati wa utawala wa Bi. Hazina Asaduzzaman Khan Kamal na maafisa waaandamizi wa ngazi za juu wa polisi.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page