![](https://static.wixstatic.com/media/146e6d_1bce415c3ef0467a8c8b5311d347152e~mv2.jpg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/146e6d_1bce415c3ef0467a8c8b5311d347152e~mv2.jpg)
Kutoka Dodoma Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Moses Nnauye pamoja na Viongozi wengine wakisalimiana na roboti aliyejitambulisha kwa jina la Eunice ambaye anakaribisha Wageni na Viongozi wanaoingia ndani ya ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma leo May 16,2024 mapema kabla ya kuwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa mwaka 2024/2025.
Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wamemleta Roboti huyu kwenye viwanja vya Bunge kwa ajili ya wabunge na wadau wa Habari kujionea teknolojia inavyozidi kukua na ubunifu wa Wizara.
Comments