top of page

WAZIRI SILAA AKABIDHI MAGARI 16




WAZIRI SILAA AKABIDHI MAGARI 16 KUTEKELEZA MRADI WA LTIP

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa amekabidhi magari 16 yenye thamani zaidi ya Shilingi bilioni 2 ambayo yatatumika kwenye Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) unaotekelezwa hapa nchini.

Waziri Silaa amesema hayo Februari 19, 2024 katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma wakati akikabidhi magari hayo kwa Katibu Mkuu ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Anthony Sanga.

"Magari haya yatumike kwa kazi ya mradi, wale wote watakaokabidhiwa magari haya wayatumie vizuri, wayatunze. Napenda kuyaona yanafanyakazi na kuongeza kasi ya utekelezaji wa uboreshaji wa milki, kazi ya matumizi bora ya ardhi vijijini na kazi ya urasimishaji katika Halmashauri mijini" amesema Waziri Silaa.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Anthony Sanga amesema Mradi huo unaotekelezwa nchini chini ya Wizara ya Adhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi unagharimu zaidi shilingi bilioni 346 ambazo ni sawa na dola za Kimarekani milioni 150.

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) Bw. Joseph Shewiyo amesema mradi huo unajukumu la kusimamia usalama wa milki za ardhi mijini na vijijini ambapo amewahamasisha wanandoa wawe na umiliki wa ardhi wa pamoja.

Mradi huo ni wa miaka mitano kuanzia 2022 hadi 2027

unatekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu

Hassan kwa kushirikiana na Benki ya Dunia.

Comentarios


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page