top of page
Radio on air

WAZIRI WA UTALII AMJULIA HALI ASKARI WA KENYA ALIYEKATIKA VIGANJA KWENYE MAANDAMANO

Taarifa kutoka nchini Kenya Waziri wa Utalii nchini humo Alfred Mutua akiwa amemtembelea na kumjulia hali Ofisa wa Polisi, David Maina ambaye alipoteza viganja vya mikono yote miwili



baada ya kitoa machozi kulipuka wakati wa maandamano yanayoendelea nchini humo.Mutua amemtembelea ofisa huyo leo Juni 20, 2024 katika Hospitali ya Nairobi West ambako anaendelea kupata matibabu baada ya kupata majeraha hayo juzi Jumanne wakati wa maandamano.

Maandamano hayo ambayo yameingia siku ya tatu leo ambapo wananchi wanapinga mapendekezo ya kuongeza kodi katika Muswada wa Fedha wa 2024 ambao uliwasilishwa bungeni Juni 18, mwaka huu.



Source: Mwananchi

Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page