top of page

WAZIRI WA ZAMANI WA FEDHA WA ERITREA AFARIKI AKIWA GEREZANI MIAKA 6 BILA HATA KUFUNGULIWA MASHTAKA

Na VENANCE JOHN


Waziri wa fedha wa zamani wa Eritrea ambaye kwa sasa alikuwa mkosoaji mkali wa rais wa nchi hiyo Berhane Abrehe amefariki akiwa gerezani.


Mzee huyo ambaye alikuwa na miaka 79 alikuwa waziri wa fedha aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi nchini Eritrea, lakini aliondolewa katika nafasi yake mwaka 2012 baada ya kutofautiana na Rais wake Isaias Afwerki. Rais Isaias ameiongoza nchi hiyo ya pembe ya Afrika, bila kufanya uchaguzi wa kitaifa, toka kushinda kwake vita vya uhuru dhidi ya Ethiopia mwaka 1991.


Baada ya miaka sita kupita, alifungwa jela kufuatia kuchapisha kitabu kilichokuwa kinaeleza kwamba rais ni dikteta hivyo ajiuzulu. Toka mwaka 2018 alikuwa akishikiliwa bila hata hivyo kupelekwa mahakamani, na mpaka anapoteza maisha bado hukumu ilikuwa haijatoka bali alikuwa rumande.


Familia imesema kuwa mamlaka, ambayo huthibitisha vifo vya maafisa wakuu waliokuwa kizuizini (jela) ndiyo iliyowapa taarifa kuhusu kifo cha Bw Berhane. Mwili wake bado haujaachiliwa, na haijabainika haswa ni muda gani umepita toka Bw Berhane afariki na kipi hasa kimepelekea Bw. Berhane kupoteza maisha.

Comentários


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page