Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Oktoba 29, 2024 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya maamuzi yafuatayo;
Ligi Kuu ya NBC
Mechi Namba 53: Young Africans SC 4-0 Pamba Jiji FC
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_e271d046427742c885507b4fa79c4b77~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_e271d046427742c885507b4fa79c4b77~mv2.jpeg)
Klabu ya Young Africans ya mkoani Dar es Salaaam imepewa Onyo Kali kwa kosa la kuchelewa kufika kwenye uwanja wa Azam Complex Oktoba 3, 2024 kuelekea mchezo tajwa hapo juu.
Yanga walifika uwanjani saa 11:10 jioni badala ya saa 11:00 jioni kwa mujibu wa Kanuni ya 17:15 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo. Adhabu hii imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 17:62 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Mechi Namba 64: Simba SC 0-1 Young Africans SC
Klabu ya Young Africans ya mkoani Dar es Salaaam imepewa Onyo Kali kwa kosa la kuchelewa kufika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Oktoba 19, 2024 kuelekea mchezo tajwa hapo juu.
Yanga walifika uwanjani saa 9:45 alasiri badala ya saa 9:30 alasiri kwa mujibu wa Kanuni ya 17:15 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo. Adhabu hii imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 17:62 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Klabu ya Yanga imetozwa faini ya Sh. 10,000,000 (milioni kumi) kwa kosa la kupitia mlango usio rasmi kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa. kuelekea mchezo tajwa hapo juu, kinyume na matakwa ya Kanuni ya 17:21 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo. Adhabu hii imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 17:62 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Klabu ya Yanga imetozwa faini ya Sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la kukataa kutumia chumba rasmi cha kuvalia kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kuelekea mchezo tajwa hapo juu, kinyume na matakwa ya Kanuni ya 17:20 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo. Adhabu hii imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 17:62 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Klabu ya Yanga imetozwa faini ya Sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la kuwakilishwa na kocha mkuu pekee kwenye mkutano wa Wanahabari kuelekea mchezo tajwa hapo juu, kinyume na matakwa ya Kanuni ya 17:58 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo inayotaka aambatane na nahodha ama mchezaji mwenye ushawishi kikosini.
Comments