top of page
Radio on air

YANGA SC YATOA POLE KIFO YUSUPH MANJI AFARIKI DUNIA

Kutoka kwenye ukurasa wa klabu ya Yanga SC imetoa taarifa hii

"Uongozi wa Young Africans Sports Club umepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha aliyewahi kuwa Mdhamini na Mwenyekiti wa Klabu yetu, Ndug. Yusuf Manji.

Kifo cha Marehemu Manji kimetokea leo, Juni 30. 2024, nchini Marekani alipokuwa akipatiwa matibabu. Rais wa Young Africans Sports Club, Eng Hersi Said amesema enzi za uhai wake



Ndugu, Yusuf Manji alikuwa kiongozi mahiri aliyejituma na kujitoa kwa ajili ya kuijenga Klabu yetu.

"Hili ni pigo kubwa kwetu Young Africans Sports Club na familia ya michezo kwa ujumla. Tutamkumbuka Yusuf Manji kwa mapenzi yake makubwa aliyokuwa nayo kwa Klabu yetu na namna alivyokuwa akijitoa kwa hali na mali katika kuiendeleza sekta ya michezo Tanzania," amesema Rais Eng, Hersi Said.

Ndugu Yusuf Manji alihudumu katika nafasi mbalimbali za kiuongozi ndani ya Klabu yetu kama Mdhamini na Mwenyekiti ambapo hadi umauti unamkuta alikuwa Mwanachama wa Young Africans Sports club.

Uongozi wa Young Africans Sports Club, unatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wanamichezo wote nchini kwa msiba mzito wa mpendwa wetu. Tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya Marehemu mahala pema Peponi, Amina. Sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea."

Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page