Na @godson2nyi
Wengi tulimfahamu kupitia kipaji chake cha kuchekesha lakini kwa kitambo sasa hatuoni tena vichekesho vyake, ila ukweli ni kwamba amejipata kwa upande mwingine kabisa wa kuwa dancer hasa baada ya kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwanadada wa kizungu Isabell ambapo kupitia uhusiano wao wanaupiga mwingi kweli kweli huko YouTube.
Ukifika huko YouTube kwa wasanii wabongo anayemfikia kwa jumla ya watazamaji (views) basi
![](https://static.wixstatic.com/media/ca9c0e_9b0ac666e22749d39b24b4917551f332~mv2.jpg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/ca9c0e_9b0ac666e22749d39b24b4917551f332~mv2.jpg)
ni Diamond Platnumz pekee sio Harmonize wala Rayvanny n.k wote wanapigwa chini kwani ana jumla ya views Bilioni 1.1 hadi sasa tunapokusogezea taarifa hii na zinaendelea kuongezeka kila uchwao. Maudhui ambayo amekuwa akiweka huko kwa sehemu kubwa ni namna wanavyospend na kucheza na mpenzi wake wakizunguka safari maeneo mbalimbali duniani ambapo video zao zimekuwa zikivutia Mamilioni ya watu kutoka pande zote za dunia.
Hii huenda imemfungulia njia kiasi cha Ukurasa rasmi wa YouTube wenye wafuasi Milioni 31 kutambua yale makubwa anayoyafanya kwenye mtandao wao hadi kumpost kwenye ukurasa wao wa Instagram na kuuliza Je unaweza kudance kama Jaymondy wakilinganisha na watu wengine maarufu kutoka mataifa ya nje hakika hili si jambo dogo.
Mbali na kutengeneza pesa nyingi mtandaoni wawili hawa pia wanapata mashavu ya ubalozi kwenye makampuni makubwa ikiwemo Coca Cola. Kila la kheri kwa JayMondy kajitafuta kajipata ila tunamiss vichekesho vyako mzee baba usitukaushie sana. Kwa leo wacha niishie hapa kalamu yangu itaandika mengine mengi wakati ujao kwa heri kwa sasa.
Comments