Kampuni ya @mziiki inayojihusisha na Usambazaji wa muziki imejibu shutma zilizotolewa na mwanamuziki Diamond Platnumz ambaye ni mmiliki wa lebo ya @wcb_wasafi kuhusu kuzuia kuachiwa kwa wimbo wa mpya "KIBANGO" wa msanij wake @iamlavalava akiwa pamoja na @diamondplatnumz ambapo barua yao imeeleza kuwa
"Tumepokea malalamiko kutoka kwenye Label ya Wasafi Juu wa kuzuia kazi ya msanii
Lavalava akishirikiana na Diamond Platnumz.
Taarifa kuhusu Release ya wimbo huo tumepokea tofauti na vile tulivyokubaliana ambapo kimkataba msanii anapaswa kuwasilisha wimbo walau week 3 kabla ya wimbo kutoka, au
![](https://static.wixstatic.com/media/ca9c0e_88b8e6f2abce4065afc3879a5b6dd31f~mv2.jpg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/ca9c0e_88b8e6f2abce4065afc3879a5b6dd31f~mv2.jpg)
kukiwa na sababu zilizo nje ya uwezo wao tunaweza kumpatia walau siku 7 ili wimbo uweze kutoka Wimbo unaolalamikiwa wa "KIBANGO", uliwasilishwa siku ya tar 16.04.2024 na kutaka utolewe siku ya tar 19.04.2024 ambapo kwa hali ya kawaida iko nje kabisa na utaratibu ulikuwa umepangwa.
Utaratibu wa utoaji wa nyimbo uko wazi na hii inaeleweka kwa wasanii wote duniani kuwa utaratibu mzuri wa kuachia wimbo kwa DSPs zote wanahitaji kusubmit nyimbo siku 21 ambayo ni sawa na wiki 3 kabla ya kutoka na sio ZiikiMedia inazuia nyimbo ya msanii, hapana. Tunaelewa kuwa kuna platform nyingi sana duniani za kusikiliza nyimbo ambazo utaratibu huu umeweka na sio ZiikiMedia.
Kila Mara tumekua tukiwaelemisha wasanii wengi hasa kutoka Tanzania juu ya utoaji kazi kwenye Digital Platforms zote, hii inaeleweka ukiachana na YouTube pamoja na local platforms kama Audiomack na Boomplay.
Tungependa kuwajuza kuwa ZiikiMedia hawajazuia Wimbo wa Lavalava & Diamond Platnumz kama inavyoelezwa na Msanii Diamond Platnumz.
Tunaamini sana kipaji na uwezo wa wasanii wetu kufanikiwa kimataifa kujenga heshima ya muziki wa Tanzania. Tunajitahidi sana kupambana na hii tunaomba wasanii washirikiane na sisi Kufikia malengo yetu kwa pamoja kwa kufuatilia taratibu za biashara ya kidigitali."Imeelezwa Ziiki.
Comments