Na VENANCE JOHN
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_b9ba675cda4b419d8b9850b4d383301c~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_b9ba675cda4b419d8b9850b4d383301c~mv2.jpeg)
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa jijini Dar es Salaam limefanikiwa kuudhibiti moto uliozuka katika jengo lenye ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) eneo la Kariakoo. Baadhi ya mashuhuda wamedai kuwa moto huo ulianza majira ya saa 6 mchana wa leo. Moto huo umeathiri sakafu (floor) moja ya jengo hilo lililo karibu na jengo la ushirika.
Hata hivyo, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limefanikiwa kuudhibiti moto huo kutoendelea kuathiri maeneo mengine. Kamishna wa mamlaka ya mapatao Tanzania (TRA) Yusuph Mwenda ni miongoni mwa waliofika eneo la tukio kufuatilia kwa karibu shughuli hiyo inavyofanyika.
Comments