top of page
Radio on air

ZUCHU ATAKA NDOA KWANZA ILI AMZALIE DIAMOND PLATNUMZ?

Hatimaye staa wa muziki wa Bongo Fleva, @officialzuchu, ameamua kutoa ya Moyoni kwa



kuweka wazi kiu yake ya kutamani kuzaa mtoto na staa wa Bongo @diamondplatnumz lakini kwa sharti la lazima wawe ndani ya ndoa.

Kupitia Insta Story Zuchu ameeleza jinsi anavyofurahi kuona Diamond anatunza na kujali watoto wake kiasi cha kupelekea jinsi hali hiyo inavyomfanya yeye kutamani kupata mtoto japo mmoja na yeye.

"Kukutazama ukiwa na watoto wako kunanifanya nitamani kuwa na mtoto na wewe", "lla ndo hivyo hujatia ubani sekhee," akimaanisha kuwa Diamond bado hajachukua hatua ya kumfanya Mama watoto wake.

Zuchu ameutumia usiku wa siku ya akina Baba hapo jana kuelezea hisia zake hizo.

Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page